UN-SYRIA

UN kuendelea kutoa misaada kwa raia wa Syria

Magari ya Umoja wa Mataifa na shirika la Msalaba Mwekundu katika mji unaoshikiliwa na waasi wa Daraya, Syria  Juni 1, 2016.
Magari ya Umoja wa Mataifa na shirika la Msalaba Mwekundu katika mji unaoshikiliwa na waasi wa Daraya, Syria Juni 1, 2016. Fadi Dirani / AFP

Umoja wa Mataifa unasema Helikopta huenda zikatumiwa kudondosha misaada ya kibinadamu kwa watu wanaoishi katika miji iliyoathiriwa na vita nchini Syria.

Matangazo ya kibiashara

Hoja hii imekubaliwa baada ya kufanyika kwa mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jijini New York nchini Marekani.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema ndege hizo zitapeleka misaada katika maeneo 15 kati ya 19 ambayo yameathiriwa na vita ikiwemo miji iliyo na watu wengi kama Allepo.

Hatua hii imekuja baada ya Mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani, Ufaransa na Uingereza kuishtuu serikali ya Syria kushindwa kutekeleza makubaliano ya kimataifa kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia raia wa kawaida.

Mamilioni ya raia wa Syria wanaishi katika mazingira magumu kwa ukosefu wa chakula, dawa na mahitaji mengine ya kibiandamu tangu kuanza kwa vita mwaka 2011 na kusababisha zaidi ya watu Laki Mbili kupoteza maisha.