SYRIA

Vikosi vya serikali ya Syria vyatekeleza mauaji ya raia kadhaa kwa mashambulizi ya anga

Vikosi vya anga vya  Syria vikishambulia maeneo yanayoshikiliwa na waasi nchini Syria
Vikosi vya anga vya Syria vikishambulia maeneo yanayoshikiliwa na waasi nchini Syria REUTERS/ECPAD/

Vikosi vya serikali ya Syria vimeua raia kadhaa kwa mashambulizi ya anga ndani na karibu na mji wa Aleppo jana Ijumaa, hata baada ya kukubali kuruhusu misafara ya kupeleka misaada kwa maeneo 12 yanayozingirwa.

Matangazo ya kibiashara

Uvamizi katika mji wa Aleppo ulikuwa makali zaidi katika kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja, na mapipa kadhaa ya mabomu na vilipuzi vimetupwa katika wilaya zinazo dhibitiwa na waasi mashariki mwa jiji, mwandishi wa AFP ameeleza.

Watu kumi na wanne wameuawa wakati basi walilokuwa wakisafiria kushambuliwa katika barabara ya Castello , barabara muhimu kwa waasi kwa ugavi nje ya Aleppo kundi la ulinzi wa raia limesema.

Takribani raia wengine 43 waliuawa katika mashambulizi yaa anga yaliyotekelezwa na serikali katika vya mji wa mashariki unaodhibitiwa na waasi limesema kundi la ulinzi wa raia linalojulikana kama White Helmets.