GENEVA-UNHCR-WAKIMBIZI

Wakimbizi milioni 65.3 mwaka 2015, rekodi mpya ya dunia

Wahamiaji wakipanda basi Machi 23, 2016 Idomeni.
Wahamiaji wakipanda basi Machi 23, 2016 Idomeni. AFP

Rekodi mpya ya dunia ilipigwa mwaka 2015, ikiwa ni pamoja na watu milioni 65.3 walioyahama makazi yao au kuzikimbia nchi zao kwa sababu ya vita na mateso, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi limetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Mwaka baada ya mwaka, tangu mwaka 2011, tarehe ya mwanzo wa mgogoro wa Syria, idadi hii inaendelea kuongezeka, kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka hivi karibuni iliyotolewa Jumatatu hii na UNHCR, wakati ambapo takwimu ilikua sawa kati ya 1996 na 2011. Ikilinganishwa na mwaka 2014, ongezeko ni 9.7%.

Watu milioni 65.3 ni zaidi ya wakazi wa Uingereza.

"Tunaishi katika dunia isiyokuwa sawa", kuna vita, migogoro na "ni vigumu kwa watu wanaotaka kwenda katika salama," Filippo Grandi, Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, amesema wakati wa kuwakilisha ripoti hii mjini Geneva, iliyochapishwa kwa ajili Siku mahsusi ya wakimbizi Duniani.

Kwa upande wake, Jan Egeland, katibu mkuu wa shirika lisilo ala kiserikali kutoka Norway la NRC, ambalo lilichangia kwa maandalizi ya ripoti hii, limebaini kwamba wakimbizi "ni waathirika wa mdororo wa usalama" kutoka kwa serikali duniani, ambazo "zinakataa kuchukua majukumu yao."

Kwa mujibu wa Bw Grandi, migogoro zaidi inayoendelea kusababisha watu wengi kuyahama makazi yao na kukimbilia uhamishoni, ni ile ile, kutoka mwaka mmoja hadi mwingine, ikiwa ni pamoja na Syria, ambayo inaongoza kwa safu ya kwanza.

Mwaka 2015 hata hivyo kuliibuka hali mpya za dharura, "Burundi, Sudan Kusini na Afghanistan."

Bw Grandi, amesema raia wa Afghanistan kwa sasa wanaunda kundi la pili la wakimbizi kwa ukubwa duniani, baada ya Syria, ambao sasa wamefikia milioni 5. "Hata raia wa Afghanistan, ambao ni wakimbizi kwa miaka mingi nchini Iran, wamekua wakielekea kwa barani Ulaya" kutafuta hifadhi, Bw Grandi ameongeza.

Miongoni mwa wakimbizi Milioni 65.3 duniani, milioni 21.3 ni wakimbizi ambao walikimbia nchini zao na milioni 40.8, ni "watu waliokimbia makazi yao" ambao hawakwenda nje ya nchi zao. Watu milioni 3.2 wanaosalia wamekua wakiomba hifadhi katika nchi ziliyostawi kiviwanda vingi.

Kwa mujibu wa UNHCR, "mtu mmoja kati ya 113 ni mkimbizi.