SAUDI ARABIA-MAREKANI

Shambulizi karibu na ubalozi wa Marekani Saudi Arabia

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Riyadh, antony Blinken alitangaza kuwa Marekani inaunga mkono muungano wa kijeshi wa Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya waasi wa Kishi wa Huthi nchini Yemen.
Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Riyadh, antony Blinken alitangaza kuwa Marekani inaunga mkono muungano wa kijeshi wa Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya waasi wa Kishi wa Huthi nchini Yemen. AFP/Ahmed Farwan

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga amejilipua Jumatatu hii karibu na ubalozi mdogo wa Marekani mjini Jeddah katika pwani ya magharibi ya Saudi Arabia, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi Arabia imetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo limetokea katika kictuo cha magari cha hospitali ya Dr Suleiman Faqeeh Jumatatu hii saa 2:15 saa za Saudi Arabia (sawa na saa 5:15 usiku saa za kimataifa Jumapili), Wizara ya Mambo ya Ndani imebaini katika taarifa yake.

Hospitali hii inapatikana karibu na ubalozi wa Marekani.

Maafisa wa usalama walijaribu kumkaribia mtu ambaye awalimshuku karibu na kituo cha magari, na wakati wakikaribia "mtu huyo alijilipua akitumia ukanda ulikua umejaa vilipuzi," Wizara ya Mambo ya Ndani imebaini.

"Lakini aliuawa. Maafisa wawili wa usalama wamepata majeraha madogo na wamelazwa hospitalini," imesema taarifa hiyo.

Mlipuko huo ulitokea Julai 4, siku ya maadhimisho ya miaka 240 ya Uhuru wa Marekani.

Hakuna mpita njia yeyote aliyejeruhiwa, lakini magari yaliyokua kwenye eneo hilo yameharibiwa.

Wachunguzi wanajaribu kujua utambulisho wa muhusika ambaye ameuawa katika shambulizi hilo, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema.

Runinga ya Saudi Arabia kwa upande wake imetangaza kwamba mlipuko huo ulitokea karibu na Msikiti.