MAREKANI-AFGHANISTAN-BARACK OBAMA

Obama atangaza kubakiza askari 8400 Afghanistan mwaka 2017

Wanajeshi wa Marekani wakipiga doria Nangarhar, tarehe 8 Septemba 2011.
Wanajeshi wa Marekani wakipiga doria Nangarhar, tarehe 8 Septemba 2011. REUTERS/Erik de Castro

Barack Obama ametangaza kubakiza nchini Afghanistan askari 8 400 mwaka 2017, na wala si 5500 kama ilivyokusudiwa hapo awali. Rais wa Marekani, ambaye alikuwa amepanga kuwaondoa askari wote wa Marekani nchini Afghanistan mwanzoni mwa muhula wake, amelazimika kurekebisha mpango wake mara kadhaa.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi unakuja baada ya uchambuzi mpya wa hali ya usalam nchini Afghanistan. Pentagon inaamini kwamba askari wa Marekani hawawezi kuendelea kuondolewa kwa kiwango kilichotangazwa miaka iliyopita na Barack Obama. Uwezekano wa vita kati ya vikosi vya Afghanistan na kundi la Taliban bado upo na vita hivi bado vinatia wasi wasi.

Mwanzoni mwa mwezi Juni, Ikulu ya White House ilikubali ya kupanua wigo wa askari wa ardhini. Bado kuna uhakika wa kuendelea kubaki nchini Afghanistan tume ya nasaha na na mafunzo kwa askari wa Afghanistan, lakini wanajeshi wa Marekani wako uhuru kuingilia kati moja kwa moja. "Kwa kubakiza askari wetu katika ngazi hii, kwa kuzingatia hali ya usalama na uwezo wa jeshi la Afghanistan, tunajipa wenyewe njia ya kutoa msaada kwa hatua hii, wakati ambapo majeshi ya Afghanistan yatakua yakiendelea kuwa imara", rais wa Marekani amesema.

Kuondolewa kwa askari wa Marekani nchini Afghanistan ni ahadi ambayo Obama hatakua ametimiza katika kipindi chote hiki cha mihula yake miwili. Rais Barack Obama anaamini kuwa mrithi wake katika Ikulu ya Marekani atkabiliana na hali hii, na kuamua kupitisha uamuzi wake wa kubakiza askari 8400 wa Marekani nchini Afghanistan.