SYRIA-IS-MASHAMBULIZI

Syria: raia 21 wauawa kwa mashambulizi ya muungano Manbij

Mpiganaji wa kundi la waasi nchini Syriaakisimama walinzi katika karibu n abarabara inayoelekea magharibi mwa mji wa Manbij katika mkoa wa Aleppo, Syria, Juni 21, 2016.
Mpiganaji wa kundi la waasi nchini Syriaakisimama walinzi katika karibu n abarabara inayoelekea magharibi mwa mji wa Manbij katika mkoa wa Aleppo, Syria, Juni 21, 2016. REUTERS/Rodi Said

Nchini Syria, kwa uchache raia 21 waliuawa Jumatatu Julai 18 katika mashambulizi ya anga ya muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani katika mji wa Manbij, ngome inayodhibitiwa na kundi la Islamic State, na kijiji jirani, kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH).

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi yalifanyika siku ya Jumatatu kwakusaidia mashambulizi ya ardhini ya wapiganaji wa Kiarabu wa Kikurdi, wanaosaidiwa na Washington, wanaojaribu kuudhibiti mji wa Manbij. Lakini tangu kuanza kwa vita hivi miezi nusu sasa dhidi ya ngome hii ya wanajihadi kaskazini mwa Syria, waasi wa Syria, waneendelea kwa mwendo wa kinyonga. Katika hatua hii, wanadhibiti tu nusu ya mji huo, ambapo maelfu ya raia wamenaswa.

Mapambano yanarindima kaskazini na magharibi mwa mji wa Manbij. Kwa mujibu wa OSDH, wapiganaji wa Kiarabu wa Kikurdi wamudhibiti mtaa mmoja Jumatatu wiki hii, baada ya mashambulizi makali ya anga ya muungano wa kimataifa, yakifuatiwa na mapigano mkali. Wanajihadi walijibu wakiendesha mfululizo wa mashambulizikatika ngome za wapiganaji wa Kiarabu wa Kikurdi, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Urusi na Syria.

Vita vya Manbij vinakumbusha vile viliyotokea katika mji wa Kobane, miaka miwili iliyopita, ambavyo viligeuka mapigano ya mitaani. Watu 104, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi haya, kwa mujibu wa OSDH.