SYRIA-UGAIDI

Syria: watu wasiopungua 44 wauawa katika shambulizi

Eneo kulikotokea shambulizi la kujitoa mhanga Qamishli, Julai 27, 2016.
Eneo kulikotokea shambulizi la kujitoa mhanga Qamishli, Julai 27, 2016. AFP

Kwa uchache watu 44 wameuawa Jumatano hii katika mji wa Syria wa Qamishli katika mji unaokaliwa na watu wengi kutoka jamii ya Wakurdi. Magaidi walioendesha shambulizi hilo wanadai kulipiza kisasi mashambulizi ya anga yanayoendeshwa na muungano unaosaidia vikosi vya Wakurdi dhidi ya makundi ya kigaidi.

Matangazo ya kibiashara

Tangu luamza kwa vita nchini Syria mwaka 2011, shambulizi hili baya kabisa limeukumba mji huu wa kaskazini mwa Syria ambapo vikosi vya Wakurdi na serikali wanagawana udhibiti.

vyombo vya habari vya serikali vimebaini kwamba "watu 44 wameuawa na wengine 140 kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na wengine kadhaa ambao wako katika hali mbaya," shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH) limebaini kwamba watu 48 wameuawa katika shambulizi hilo.

Shambulio hili la kujitoa mhanga, lililotekelezwa kwa kutumia gari lililokua limetegwa bomu, limetokea katika sekta ya magharibi ya Qamishli ambapo kunapatikana vyombo vya usalama vya utawala wa Wakurdi, kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.

Mji wa Qamishli umeendelea kukumbwa na mashambulizi mbalimbali ya kujitoa mhanga.

Wakati huo huo muungano wa kimataifa unaopambana dhidi ya makundi ya kigaidi wamesema Jumatano hii kwamba wameanzisha uchunguzi ili kujua kama mashambulizi yake ya wiki iliyopita, karibu na mji wa Minbej yaliasababisha majeruhi upande wa raia.