UN-YEMEN

Yemen yaridhia mkataba wa amani wa UN

Serikali ya Yemen imesema hii leo kuwa imeridhia pendekezo la mkataba wa amani la UN ili kumaliza mzozo wa zaidi ya mwaka mmoja ingawa upande wa waasi haujatoa kauli yoyote.

Baadhi ya Viongozi wa wapiganaji wanaounga mkono serikali ya Yemen mjini Taëz, nchini Yémen, le 18 juin 2016.
Baadhi ya Viongozi wa wapiganaji wanaounga mkono serikali ya Yemen mjini Taëz, nchini Yémen, le 18 juin 2016. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Tangazo la serikali inayoungwa mkono na saudia arabia linakuja baada ya mkutano wa viongozi huko Kuwait uliosimamiwa na raisi wa Aberabbo Mansour Hadi.

Mkutano huo umeidhinisha rasimu ya pendekezo la umoj awa mataifa lililotaka kukomeshwa kwa uhasama na kuondoka kwa waasi mjini sanaa na katik amiji ya Taez na Al-Hudaydah,kwa mujibu wa shirika la habari SABA.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Yemen Abdulmalek al-Mikhlafi,ambaye anaongoza jopo la wajumbe wa serikali katika majadiliano amesema kuwa amemuandikia barua mjumbe maalum wa UN kumtaarifu kuwa serikali inaunga mkono makubaliano yaliyofikiwa nchini kuwait.

Hata hivyo upande wa waasi haujatoa kauli yoyote.