Pata taarifa kuu
PAKISTAN-TALIBAN-MAUAJI-MASHAMBULIZI

Watu wasiopungua 20 wauawa katika shambulio kusini magharibi mwa Pakistan

Mashia karibu na miili ya watu waliouawa karibu Februari 16 katika mashambulizi yaliyotokea katika mkoa wa Quetta, Februari 19, 2013.
Mashia karibu na miili ya watu waliouawa karibu Februari 16 katika mashambulizi yaliyotokea katika mkoa wa Quetta, Februari 19, 2013. REUTERS/Naseer Ahmed
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Kwa uchache watu ishirini wameuawa katika shambulio la bomu dhidi ya hospitali katika mkoa Quetta, mji mkuu wa jimbo lyenye utata la Baluchistan kusini magharibi mwa Pakistan, mpiga picha wa shirika la habari la AFP, amesema.

Matangazo ya kibiashara

Wengi wa wahanga ni wanasheria na waandishi wa habari waliokuwa wamekusanyika muda mfupi kabla juu ya tukio la maandamano dhidi ya mauaji ya Mwenyekiti wa chama cha wanasheria mkoa huo, chanzo hicho kimesema.

Mwezi Machi shambulizila la kujitoa mhanga lilitokea katika hifadhi ya manispa ya jiji la Lahore, Jumapili ya Pasaka, na liliwaua watu wasiopungua 72.

Watoto walikuani miongoni mwa wahanga waliouawa katika shambulizi hilo ambalo ni pigo kubwa kwa matumaini ya kuboresha usalama.

Shambulizi hili lilidaiwa kutekelezwa na kundi la Taliban nchini Pakistan, ambalo lilisema lilikua limeilenga jumuiya ya kikristo. Lakini kwa mujibu wa Naibu mkuu wa Polisi Haider Ashraf, wengi wa wahanga walikua Waislamu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.