SYRIA-VITA

Syria: vita muhimu Aleppo, Umoja wa Mataifa watiwa hofu kwa raia

Askari wa jeshi la serikali  ya Syria wanakikagua silaha zilizoachwa na wapiganaji wa kundi la Islamic State katika jimbo la Aleppo, Novemba 20, 2015.
Askari wa jeshi la serikali ya Syria wanakikagua silaha zilizoachwa na wapiganaji wa kundi la Islamic State katika jimbo la Aleppo, Novemba 20, 2015.

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa misaada ya haraka kwa takriban watu milioni 1.5 katikamji wa Aleppo ambapo mapigano kati ya serikali na waasi, yanaonekana kuandaliwa zaidi kwa ajili ya vita muhimu kwa udhibiti wa mji wa pili wa Syria.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Syria inaungwa mkono na ndege za Urusi na wapiganaji wa Iran, Iraq na wale wa Hezbollah kutoka Libanon, na makundi ya waasi yanaungwa mkono nakundi kubwa la kijihadi la Fateh al-Sham (kundi la zamani la Al-Nosra Front lililojitenga na kundi la Al-Qaeda).

Pande zote mbili wamepokea reinforcements muhimu katika wanaume na silaha katika Aleppo na viunga vyake baada ya waasi kuvunja Jumamosi ya wiki tatu ya kuzingirwa zilizowekwa na serikali kwa maeneo wanayoyadhibiti katika mji wa kaskazini kugawanywa tangu 2012.

Kutokana na hali hiyo, waasi wameweza kuzingira sehemu moja ya maeneo yanayoshikiliwa na jeshi la serikali,magharibi mwa jimbo la Aleppo kabla ya kutangaza nia yao ya kuuteka mji mzima, suala kubwa la migogoro unaoiathiri nchi hiyo kwa zaidi ya miaka mitano.

Mamia ya maelfu ya askari na raia sasa wako katika mji wa Aleppo wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali mahitajio, na hivyo kusababisha Umoja wa Mataifa kuwa na hofu.

"Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia raia katika mji wa Aleppo, mji ambao unakumbwa matatizo mbalimbali," Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Yacoub El Hillo, na Mratibu wa kikanda, Kevin Kennedy wamethibitisha.

Kama Umoja wa Mataifa unatambua ukubwa wa tatizo hili, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limegawanywa kuhusu masharti yanayotakiwa kabla ya kutuma msaada.

Marekani na Ufaransa waliosema Jumanne hii kwamba misaada inapaswa kuwasili mjini Aleppo kabla ya mazungumzo mapya ya amani yaliyopangwa kufanyika hivi karibuni.

Hata hivyo, Urusi imeendelea na msimamo wake kwamba masharti hayana nafasi kwa mazungumzo hayo, Umoja wa Mataifa una matumaini ya kuanza tena kwa mazungumzo mjini Geneva mwishoni mwa mwezi huu.