UN-SYRIA

Baraza la usalama la UN kujadili mzozo wa Syria

Mashambulizi yameendelea kuripotiwa jijini Aleppo ambapo raia wanatajwa kupoteza maisha.
Mashambulizi yameendelea kuripotiwa jijini Aleppo ambapo raia wanatajwa kupoteza maisha. AMEER ALHALBI / AFP

Baraza la usalama la umoja wa mataifa linataraji kukutana leo jumapili kujadili mzozo wa Syria ambao unaendelea kutokota katika jiji la Aleppo,wanadiplomasia wamesema.

Matangazo ya kibiashara

Kikao hicho cha leo kimeitishwa na Uingereza,Ufaransa,na Marekani.

Makabiliano makali yameendelea na kuua takribani raia arobaini na tano mjini Aleppo ikiwa ni siku mbili baada ya jeshi la Syria kutangaza kufanya mashambulizi kudhibiti mji unaokaliwa na waasi katika upande wa mashariki.

Katibu mkuu wa UN Ban Ki-moon amelaani mapigano hayo na kuonya kuwa matumizi ya silaha kali yatasababisha uhalifu wa kivita.

Ban alikariri ripoti za mashambulizi ya anga na matumizi ya silaha za hali ya juu katika makabiliano yaliyoanzishwa na vikosi vya Syria siku mbili zilizopita likilenga kurejesha udhibiti wa mji unaoshikiliwa na waasi.