UN-SYRIA

Raia 23 wauawa Aleppo Syria

Takribani raia ishirini na tatu wameuawa katika siku moja ya mashambulizi ya papo kwa papo kutekelezwa na vikosi vya serikali Urusi na vikosi vinavyoipinga serikali ya Assad.

Mashambulizi yameendelea mjini Aleppo na kushudia hali ya sintofahamu
Mashambulizi yameendelea mjini Aleppo na kushudia hali ya sintofahamu KARAM AL-MASRI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na ndege za kivita ambazo hazikutambulika za vikosi gani zilisababisha vifo kumi na mbili vya raia jana ijumaa katika eneo la upinzani mashariki mwa Aleppo,kwa mujibu wa shirika la waangalizi wa haki za binadamu.

Mashambulizi hayo yanaaminiwa kufanywa na ndege za jeshi la Syria na mshirika wake Urusi na kutibua hali ya kibinadamu mashariki mwa Aleppo.

Wakati huu vikosi vya Syria vikisonga mbele jimboni Aleppo kwa kusaidiwa na mashambulizi ya anga ya Urusi,shirika la madaktari wasio na mipaka limesema eneo la mapigano linalokaliwa na waasi mashariki limegeuka dimbwi la damu.

Syria inasonga mbele wakati huu mazungumzo kati ya wadau wa vita hivyo Urusi na Marekani yakionekana kukwama.