AFGHANISTAN-WAKIMBIZI

Suala la wakimbizi wa Afghanistan kujadiliwa katika mkutano wa Brussels

Nchi sabini na mashirika ishirini ya kimataifa vimelialikwa katika mkutano kuhusu Afghanistan ambao unaanza Jumatatu hii Oktoba 3 mjini Brussels. Rais Ashraf Ghani atawasilisha mpango wa serikali yake kwa jumuiya ya kimataifa. Pia atatoa ahadi za mageuzi mapya akiwa matumaini ya kupata msaada mkubwa. Lakini nchi hii bado iko katika vita, na bado ni moja ya mataifa maskini katika ukanda huo.

Wakimbizi wa Afghanistan wakikaa chini ya daraja karibu na mji wa Ventimiglia, mji wa Italia kwenye mpaka wa Ufaransa na Italia, mwezi Septemba 2016.
Wakimbizi wa Afghanistan wakikaa chini ya daraja karibu na mji wa Ventimiglia, mji wa Italia kwenye mpaka wa Ufaransa na Italia, mwezi Septemba 2016. RFI/Géraud Bosman-Delzons
Matangazo ya kibiashara

Raia wengi wa Afghanistan wanaikimbia nchi yao na kuingia Ulaya. Raia wa Afghanistan wanawakilisha kundi la pili kwa wingi wa wakimbizi kuwasili barani Ulaya baada ya Syria. Suala nyeti la kurudi kwa wakimbizi wa Afghanistan katika nchi zao litajadiliwa katika mkutano huu unaotazamiwa kufanyika mjini Brussels Jumatatu hii.

"Ni wakati wakimbizi wa Afghanistan walianza kuwasili barani Ulaya na wakimbizi wengine ndipo jumuiya ya kimataifa,ghafla, ilipata taarifa ya kuwepo kwa wakimbizi hao." Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi Filippo Grandi alisema mwezi Juni.

Raia wa Afghanistan waliikimbia nchi yao toka zamani, hali iliyosababishwa, mwishoni mwa miaka ya 1970, na mapinduzi ya kikomunisti, kisha uvamizi wa kikosi cha Red Army, na kuzuka kwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kati ya mwaka 2002 na 2008 wakati utawala wa Taliban unaangushwa mamilioni ya raia wa Afghanistan walirejea nyumbani kwa kujenga upya nchi yao.

Hali hii inasababisha ujenzi wa taifa hili kuchelewa, na vurugu zimeongezeka tangu kuondoka kwa kikosi cha kimataifa mwishoni mwa mwaka 2014, hali iliyosababisha raia wengi kuikimbia nchi hiyo.

Majirani zao (Iran, Pakistan) hawakubali kuwapokea, na hivyo wanajaribu kwenda Ulaya. Kati ya mwezi Januari na mwezi Desemba 2015, Waafghanistan 200,000 waliomba hifadhi ya ukimbizi katika nchi moja ya Ulaya, idadi hii ikiwa ni mara sita zaidi ya ile ya mwaka 2014 .

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uingereza, Umoja wa Ulaya ulikua umepanga kuishinikiza serikali ya Afghanistan kukubali kurundi kwa wahamiaji 80 000 huku ikitishia kusitisha misaada.