SYRIA-USALAMA

Jeshi la Syria latangaza 'kupunguza' mashambulizi yake katika mji wa Aleppo

Uharibifu unaosababishwa na mashambulizi ya anga katika mji wa Aleppo, Februari 27, 2016.
Uharibifu unaosababishwa na mashambulizi ya anga katika mji wa Aleppo, Februari 27, 2016. Reuters

Jeshi la Syria limetangaza Jumatano hii kwamba 'litapunguza' mashambulizi yake ya anga katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi katika mji wa Aleppo, kaskazini mwa nchi. Jeshi la Syria linasema limechukua uamuzi huo baada vikosi vya serikali kusonga mbele katika mji huo unaolengwa kwa wiki mbili na mashambulizi makali.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya mafanikio ya majeshi yetu katika mji wa Aleppo na kufunga barabara zote zinazotumiwa kwa kuingiza chakula kwa upande wa makundi ya kigaidi, amri imetolewa ya kupunguza idadi ya mashambulizi ya anga na makombora kwenye ngome za magaidi, "jeshi limebaini katika taarifa yake irushwa na vyombo vya habari vya serikali.

Taarifa hii pia inabaini kuwa uamuzi huo ulichukuliwa ili 'kuruhusu raia ambao wanataka kuondoka eneo hilo na kwenda maeneo salama.'

Jeshi lilitangaza tarehe 22 Septemba kuwa linaanzisha mashambulizi makali kwa minajili ya kuyaweka kwenye himaya yake maeneo yanayoshikiliwa na waasi katika mji wa Aleppo, ambao umegawanyika tangu mwaka 2012 kati ya eneo la magharibi linaloshikiliwa na serikali na eneo jingine linalodhibitiwa na waasi

Pamoja na msaada mkubwa wa ndege za kivita za Urusi, vikosi vya serikali vimesonga mbele katikati, kaskazini na kusini mwa mji mkuu wa zamani wa kiuchumi wa Syria.