IRAQ-UTURUKI-MVUTANO

Serikali ya Iraq yalalamikia jeshi la Uturuki

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likipigia kura kwa kauli moja azimio azimio linalolenga kushambulia wanajihadi wa kundi la Islamic State, mjini New York tarehe 17 Desemba mwaka 2015.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likipigia kura kwa kauli moja azimio azimio linalolenga kushambulia wanajihadi wa kundi la Islamic State, mjini New York tarehe 17 Desemba mwaka 2015. REUTERS/Mike Segar

Serikali ya Iraq imeomba kufanyika kwa mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kujadili uwepo wa vikosi vya Uturuki kaskazini mwa Iraq, runinga ya taifa nchini Iraq imearifu Alhamisi wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Haidar al Abadi alikuwa amesema siku moja kabla hatari ya vita kwa sababu ya kutumwa kwa askari hao, ambapo muda wao uliongezwa kwa mwaka mmoja, wiki iliyopita na Bunge la Uturuki. Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq ilimuitisha balozi wa Uturuki Jumatano wiki hii kumpa taarifa ya kupinga hali hiyo, jitihada kama hiyo ilichukuliwa na serikali ya Ankara.

Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yildirim amesema 'kutoelewa' msimamo wa serikali ya Baghdad kwa kuwepo kwa askari wa Uturuki katika kambi ya Bachika, kaskazini mwa mji wa Mosul.

Uturuki inasema kuwa ilituma askari wake mwishoni mwa mwaka jana kwa mwaliko wa Massoud Barzani, rais wa mkoa unaojitegemea wa Kurdistan nchini Iraq kama sehemu ya ujumbe wa kozi na mafunzo ya vikosi vinavyopambana dhidi ya wanajihadi wa kundi la Islamic State (IS).

Yildirim, akizungumza Alhamisi mbele ya wafanyabiashara, amesema kuwa askari wa Uturuki wangelibaki eneo hilo ili kuhakikisha utulivu kwa watu wote wa ukanda huo.

Serikali ya Baghdad, ambayo imezungumzia uwepo wa askari 2,000 wa Uturuki, inaamini kwamba askari hao ni kikosi cha uvamizi.

Mvutano kati ya Ankara na Baghdad unatokana na maandalizi kwa ajili ya vita vya kudhibiti Mosul, mji wa pili nchini Iraq unaodhbitiwa na wanajihadi wa kundi la Islamic State tangu mwezi Juni 2014.