SYRIA-USALAMA

Watu zaidi ya 20 wauawa katika shambulio karibu na mpaka wa Uturuki

Bab al-Salama, katika mpaka wa Syria na Kituruki. Ni wakati wa sala kwa waasi wa Syria ambao wanadhibiti eneo hilo.
Bab al-Salama, katika mpaka wa Syria na Kituruki. Ni wakati wa sala kwa waasi wa Syria ambao wanadhibiti eneo hilo. REUTERS/Umit Bektas

Kwa uchache watu 20, wengi wao wakiwa wapiganaji wa makundi ya waasi nchini Syria waliuawa Alhamisi katika mlipuko wa bomu lilitegwa katika gari karibu na mpaka wa Bab al Salam, kwenye mpaka na Uturuki, kaskazini mwa Syria, mashahidi wawili wamesema.

Matangazo ya kibiashara

Mashahidi hawa wanasema kwamba mlipuko ulitokea karibu na kituo cha ukaguzi kinachodhibitiwa na waasi kundi la Free Syrian Army, kilomita mbili kutoka karibu na mpaka na Uturuki.

Watu kadhaa waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali ya Azaz, shahidi mmoja ameeleza, na kuongeza kwamba misikiti imekua ikitolea wito raia kuchangia kwa damu.

Kwa uchache watu 25 walijeruhiwa, wanane wako katika hali mbaya. wanne hawa walipelekwa katika hospitali nchini Uturuki, upande wa pili wa mpaka.

Wiki moja iliyopita, mpiganaji wa kundi la Islamic State alijilipua kwenye mpaka wa Athmeh, katika mkoa wa Idlib na kuua watu 25, wenye uhusiano nakundi la wasi la Free Syrian Army.