KUWAIT-SIASA-UCHUMI

Bunge la Kuwait lavunjwa katika hali ya mvutano wa kisiasa

Kiongozi wa nchi ya Kuwait, Sheikh Sabah al-Ahmad al-Jaber al-Sabah, Mei 27, 2015.
Kiongozi wa nchi ya Kuwait, Sheikh Sabah al-Ahmad al-Jaber al-Sabah, Mei 27, 2015. AFP / Yasser Al- Zayyat

Kiongozi wa nchi ya Kuwait, Sheikh Sabah al-Ahmed al-Sabah, amevunja Jumapili hii Bunge la nchi hii tajiri kwa mafuta katika ukanda wa Ghuba baada ya mvutano kati ya wabunge na serikali kuhusu hatua kali zinazochukuliwa na serikali.

Matangazo ya kibiashara

Amri ya kiongozi wa Kuwait ilizua 'utata' na "changamoto za usalama" katika ukanda huo kwa kuhalalisha uamuzi wa kuvunja Bunge, bila hata hivyo kujali mvutano wa ndani wa kisiasa nchini humo.

Kuwait, nchi ya kwanza ya Ghuba kuwa na Bunge tangu miaka ya 1960, inakabiliwa na mgogoro wa kisiasa, hali ambayo imezuia mageuzi mbalimbali ya kiuchumi.

Kushuka kwa bei ya mafuta pia kunaathiri uchumi wa nchi hii, ambayo n imwanachama wa Shirika la Nchi zinazouza mafuta (OPEC).

Kuwait imeshuhudia nakisi ya bajeti ya Dinar bilioni 4.6 (sawa na Euro bilioni 13.7) katika mwaka wa fedha uliopita ambao ulimalizika Machi 31, baada ya miaka 16 ya ziada kutokana na bei ya juu ya dhahabu nyeusi.

Nchi hii ina wakazi milioni 1.3, ambapo 30% ni watu kutoka jamii ya Mashia na baadhi ya watu milioni tatu ambao ni raia wa kigeni waishio nchi humo.