AFGHANISTAN-MAREKANI-USALAMA

Afisa wa juu katika jeshi la Marekani akosoa majeshi ya Afghanistan

AFP

"Amri zenye dosari" katika uongozi wa vikosi vya polisi na jeshi la Afghanistan zimesababisha idadi ya waathirika kuongezeka katika vikosi vya serikali, ambebaini Jumapili hii afisaa mkuu wa jeshi la Marekani, jenerali John Nicholson, mkuu wa majeshi ya NATO nchini Afghanistan.

Matangazo ya kibiashara

"Tuna wasiwasi mkubwa na kiwango cha juu cha waathirika," amewaambia waandishi wa habari afisa pia anayeongoza vikosi vya Marekani nchini Afghanistan na kusema kuwa bado wanasubiri hasara' kubwa pia", labda ilio juu zaidi ikilinganishwa na ile ya mwaka 2015, kwa mujibu wa vitengo mbalimbali vya vikosi hivyo na mikoa.

Mwaka jana, zaidi ya askari na polisi 5,000 wa Afghanistan waliuawa na wengine 15,000 kujeruhiwa katika mapambano dhidi ya wapiganaji wa Taliban.

"Moja ya sababu kuu ya kiwango hiki cha juu cha waathirika, ni uongozi. Amri zenye dosari katika ngazi mbalimbali za uongozi. Ukianzia polisi na kwa kiasi kidogo katika jeshi, " jenerali Nicholson amebaini.

"Maafisa hawa vijana wa polisi ambao wanakufa katika vituo vya ukaguzi hawana chakula cha kutosha wala maji ya kutosha au risasi za kutosha, na wasimamizi katika jeshi wanakua hawako pamoja nao," ameongeza jenerali Nicholson, huku akilaani rushwa ndani ya Wizara ya Mambo ya.

Zaidi ya askari 12,000 kutoka nchi za Magharibi, ikiwa ni pamoja askari 10,000 kutoka Marekani, wametumwa nchini Afghanistan chini ya Operesheni ijulikanayo kwa jina la Resolute Support, kwa kutoa mafunzo na kusaidia majeshi ya Afghanistan dhidi ya wapiganaji wa Kiislam.