UN-SYRIA

Ban;Baraza la usalama liombe ICC ichunguze uhalifu wa kivita nchini Syria

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon amelaani shambulizi lililolenga shule katika eneo linalodhibitiwa na serikali magharibi mwa Aleppo ambalo liliua watoto kadhaa wa Syria.

Mashambulizi yameendelea kuripotiwa jijini Aleppo ambapo watu wanatajwa kupoteza maisha.
Mashambulizi yameendelea kuripotiwa jijini Aleppo ambapo watu wanatajwa kupoteza maisha. KARAM AL-MASRI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ban amesema huenda mashambulizi hayo yakawa uhalifu wa kivita.

Vyombo vya habari nchini Syria vimeripoti makombora ya waasi yalilenga shule huko Aleppo ambapo jiji limegawanyika tangu katikati mwa mwaka-2012, baada ya waasi kudhibiti eneo la mashariki mwa Mji.

Shirika la habari SANA limeripoti watoto watatu waliuawa na wengine 14 kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi katika shule ya Shahba huko Aleppo.

Katibu mkuu Ban Ki Moon amerejelea wito wake kwa baraza la usalama kuiomba mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kuchunguza madai ya uhalifu wa kivita nchini Syria.