SAUDI ARABIA-IS-USALAMA

Saudi Arabia yatangaza kuzima shambulizi la IS

Magari ya polisi ya Saudi arabia yakiegeshwa katikati ya mji wa Riyadh. Vikosi vya usalama iko makini kwa tishio makundi ya kijihadi.
Magari ya polisi ya Saudi arabia yakiegeshwa katikati ya mji wa Riyadh. Vikosi vya usalama iko makini kwa tishio makundi ya kijihadi. AFP PHOTO/FAYEZ NURELDINE

Serikali ya Saudi Arabia imetangaza Jumapili hii kwamba imefaulu kuvunja makundi mawili ya 'magaidi' wanaohusiana na kundi la Islamic State (IS), ambapo kundi moja lilipanga shambulizi wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia-2018 katika mji wa Jeddah.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa wizara mambo ya ndani ya Saudi Arabia, wanajihadi wanane kutoka makundi hayo mawili wamekamatwa.

Wanachama wa kundi la kwanza wanaishi katika mkoa wa Shaqra (katikati mwa nchi), ni raia waane kutoka Saudi Arabia. Kundi hili limekua likipokea amri ya afisa wa kundi la IS nchini Syria na lilikua linataka kulenga vikosi vya usalama katika mji mkuu wa nchi hii, Riyadh katika mji wa Tabuk (kaskazini magharibi) na mashariki ya ya Saudi Arabia, wizara ya mambo ya ndani imeshtumu. Raia wengine sita kutoka Saudi Arabia wamekamatwa na wamehojiwa kuhusu uhusiano wao na kundi hilo.

Kuhusu kundi la pili, raia wawili kutoka Pakistan, mmoja kutoka Syria na mmoja kutoka Sudan walikuwa wamepanga kutekeleza shambulizi la bomu lililotegwa katika gari kwenye moja ya vituo vya magari kwenye uwanja mmoja wa mpira mjini Jeddah, siku ya mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia-2018, Oktoba 11. Mechi hii ilikua kati ya Saudi Arabia Falme za Kiarabu.

Julai mwaka jana, serikali ya Riyadh ilitangaza kwamba iliwakamata watuhumiwa 19, ikiwa ni pamoja na raia 12 kutoka Pakistani, kwa mashambulizi ya kujitoa mhanga, ikiwa ni pamoja shambulizi la kipekee katika mji wa Madina, mji wa pili mtakatifu kwa takatifu kwa Waislamu, na lile lililotekelezwa karibu na ubalozi mdogo wa Marekani mjini Jeddah.