SYRIA-USALAMA
Mapiganao yaendelea kurindima katika mji wa Allepo
Jeshi la Syria na wapiganaji wa upinzani wameendelea kupambana katika mji wa Allepo na kusababisha vifo vya watu 41 kwa muda wa siku tatu zilizopita.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Wanaharakati wa haki za Binadamu wanasema miongoni mwa watu waliopoteza maisha ni watoto 17.
Wakati makabiliano hayo yakiendelea, serikali ya Syria imewashtumu waasi wa kwa kurusha mabomu yenye gesi katika ngome ya wanajeshi wake.
Staffan de Mistura Msuluhishi Mkuu wa mzozo huu amelaani mashambulizi hayo anayosema wanawauawa raia wasiokuwa na hatia.