MAREKANI-URUSI-SYRIA-USHIRIKIANO

Kremlin yawasiliana na timu ya Trump juu ya Syria

Ofisi ya rais wa Urusi (Kremlin) imeanzisha mawasiliano na timu iliyoundwa hivi karibuni na Rais Mteule wa Marekani Donald Trump kuhusu hali nchini Syria, Naibu Waziri wa Urusi, Mikhail Bogdanov, ametangaza Alhamisi hii.

Rais wa Urusi Vladimir Putin ana matumaini ya kushirikiana vema na utawala ujao wa Marekani.
Rais wa Urusi Vladimir Putin ana matumaini ya kushirikiana vema na utawala ujao wa Marekani. REUTERS/Sergei Karpukhin
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Urusi, Bw. Bogdanov amesema kuwa Urisi ina matumaini kwamba utawala ujao wa Marekani utapitisha utaratibu mpya kuhusu Syria.

Vladimir Putin na Donald Trump walizungumza kwa njia ya simu siku ya Jumatatu wiki hii katika jitihada za rais wa Urusi, na walikubaliana kuzungumza "katika kuheshimiana" na kujitahidi "kujenga ushirikiano", kwa mujibu wa taarifa ya Kremlin.

Wawili hao, Ofisi ya rais wa Urusi imeongeza, walikubaliana kwa kuweka pamoja juhudi zao za kupambana na ugaidi na msimamo mkali na kuamua kuweka kuwasiliana mara kwa mara wakati ambapo wakiandaa mkutano wao wa kwanza.

Mjini Washington, timu yaRais Mteule wa Marekani imesema kuwa Donald Trump, ambaye atachukua hatamu ya uongozi wa nchi Januari 20, alikuwa alionyesha nia yake ya kuanzisha ushirikiano wa kudumu na Urusi pamoja na raia wake.