MAREKANI-JORDAN

Vifo vya maafisa watatu wa CIA nchini Jordan vyaibua maswali mengi

Mfalme Abdullah II wa Jordan, mjini Amman Novemba 7, 2016 mbele ya askari wake.
Mfalme Abdullah II wa Jordan, mjini Amman Novemba 7, 2016 mbele ya askari wake. Yousef ALLAN / AFP Jordanian Royal Palace / AFP

Askari mmoja wa Jordan ambaye aliwaua wakufunzi watatu wa CIA Novemba 4, naweza kuwa aliongozwa na itikadi za kigaidi. Habari hii iligonga vichwa vya habari katika siku za hivi karibuni nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Askari wa Jordan alifyatua risasi dhidi ya msafara wa magari ya kijeshi yaliyokua yakiingia katika kambi ya jeshi la kikosi cha wanaanga cha Jordan kusini mwa nchi hiyo. Uchunguzi bado unaendelea, hakuna hitimisho lolote rasmi. Kesi hiyo inaisakama Jordan

Masaa machache kabla ya tukio hilo, Ijumaa, Novemba 4, serikali ya Jordan ilitangaza kuwa msafara wa magari ya kijeshi ulikuwa ukijaribu kuingia katika kambi ya kikosi cha wanaanga bila kusimama ili uweze kukaguliwa. Wakati huo huo askari wa Jordan alifyatua risasi dhidi ya msafara huo.

Madai hayo yalipingwa na Marekani, na serikali ya Jordan mara moja ilibadili maelezo yake. "kulisikika milio ya risasi katika msafara wa magari ya kijeshi; na askari wa Jordan aliye kuwa katika ulinzi alijibu akiamini kwamba ni shambulio, " serikali ya Jordan imesema.

Kauli nyingine

Serikali ya Jordan hatimaye imetangaza kwamba tukio lililotokea dhidi ya magari ya kijeshi na kusababisha vifo vya maafisa watatu wa CIA lilikua shambulio la kigaidi. Kauli hii huenda ikawekwa hatarini na vyombo vya habari vya Marekani. Gazeti la New York Times limemuhoji mmoja wa askari walionusurika katika shambulio hilo.

Askari huyu ambaye bado kijana aliweka mambo wazi, akisem akwamba hakuna chochoko iliyokanzishwa na upande wa kundi lake. "Askari hawakuwa na kitu chochote ispokua ispokua bastola tu. Na walikuwa wakirudi kutoka kwenye mafunzo," amesema askari huyo.

Mshambuliaji mkuu bado yuko hai. Alijeruhiwa vibaya, lakini anapaswa kueleza nia yake, Ubalozi wa Marekani mjini Amman umesema katika taarifa yake.