SYRIA-USALAMA

Vita nchini Syria: Ufaransa yaandaa mkutano mpya mjini Paris

Mashambulizi ya anga yaendelea kurindima katika mji wa Aleppo, nchini Syria
Mashambulizi ya anga yaendelea kurindima katika mji wa Aleppo, nchini Syria REUTERS/Abdalrhman Ismail

Ufaransa itazikutanisha mapema mwezi Desemba mjini Paris nchi za Magharibi na zile za Kiarabu ambazo zinaunga mkono upinzani wenye msimamo wa wastani nchini Syria, wizara ya mambo ya nje ya ufaransa imetangaza Jumatano hii baada ya kikao cha baraza la mawaziri.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu utawakutanisha Mawaziri wa mambo ya Nje wa Marekani, nchi za Ulaya, Uturuki na nchi kadhaa za Kiarabu.

Hayo yakijiri mashambulizi ya anga yameendelea kushuhudiwa katika mji wa Aleppo ambapo wakazi wa mji huo wamendelea kuishi kwa hofu. Mashambulizi haya yamekua yakiendeshwa na vikosi vya Syria na washirika wao, huku kukiarifiwa janga la kibinadamu na matumizi ya silaha za kemikali yameelezwa wiki iliyopita na wataalam waliotumwa na Umoja wa Mataifa, jambo ambalo limepelekeaWaziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, kuchukua msimamo kwa mara yingine tena. Mwishoni mwa mwezi Mei Ufaransa ilikuwa tayari kuanzisha mkutano kuhusu mgogoro wa Syria.

"Tunakabiliwa na vita sehemu zote, vita abavyo kwa sasa vimewakatisha tamaa wakazi wa mji wa Aleppo, ambao wanakadiriwa kufiki 300,000. Hakuna hospitali hata moja, watoto wachanga wamekua wakilazimika kuondolewa maeneo ambao wamekua wakihudumiwa kimatibabu. Huo ndio ukweli. Swali linakuja ni kujua iwapo mataifa hayo yatatofautiana kuhusu utaratibu wa kutumia? Ufaransa haitokubali kuwepo na tofauti na Ufaransa si chanzo cha tofauti. Iko tayari kushiriki, " amesema Waziri Jean-Marc Ayrault.

"Leo kuna watu milioni moj ambao wamezingirwa, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa. Si tu katika mji wa Aleppo lakini pia katika miji ya Homs, Ghouta, Idleb ... Huu ni ukweli wa hali ya mambo nchini Syria leo, " Bw. Ayrault ameongeza.

Ndege za kivita za Urusi zikiruka kutoka chombo cha majini cha Urusi kiitwacho Amiral Kuznetsov, kikipiga kambi katika pwani ya Syria, Novemba 15, 2016.
Ndege za kivita za Urusi zikiruka kutoka chombo cha majini cha Urusi kiitwacho Amiral Kuznetsov, kikipiga kambi katika pwani ya Syria, Novemba 15, 2016. Ministry of Defence of the Russian Federation/Handout via REUTER

Nchi "marafiki wa demokrasia nchini Syria"

"Nimechukua hatua ya kukutanisha mjini Paris katika siku zijazo nchi rafiki wa demokrasia nchini Syria, upinzani wenye unaotaka kudumu kwa demokrasia nchini Syria," amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa ambaye amezitaja nchi zilizoalikwa katika mkutano huo: Ufaransa, Ujerumani, Italia, Uingereza, Marekani, nchi za Kiarabu, kama Saudi Arabia, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu, Jordan, na Uturuki.

"Ni muhimu jumuiya ya kimataifa kuacha kufumbia macho hali hii inayoshuhudiwa nchini Syria. Ni ukweli unaotisha unaotokea nchini Syria, na ni haraka kuchukua hatua, " Bw. Ayrault amesema akisisitiza.