SYRIA-USALAMA

Jeshi la Syria lawatimua waasi mjini Allepo

mashambulizi ya anga kwenye eneo la waasi la Al-Sakhour katika mkoa wa Allepo, Novemba 29, 2016.
mashambulizi ya anga kwenye eneo la waasi la Al-Sakhour katika mkoa wa Allepo, Novemba 29, 2016. REUTERS/Abdalrhman Ismail

Jeshi la Syria limefanikiwa kuwaondoa waasi katika ngome yao Kaskazini mwa mji wa Allepo. Jumatatu hii, Novemba 28, kitongoji cha al-Sakhour kimewekwa chini ya udhibiti wa vikosi vya serikali. Hili ni pigo kubwa kwa waasi wa Syria, baada y kuonekana kuzidiwa nguvu na jeshi la serikali na kupoteza maeneo kadhaa.

Matangazo ya kibiashara

Serikali hii Damascus inasema hatua hii ni muhimu na jeshi linaelekea kudhibiti mji wote ambao umekuwa ngome ya waasi hao.

Maelfu ya wakaazi wa mji huo wamekuwa wakiondoka wengine wakielekea Kusini mwa mji huo eneo ambalo bado linadhibitiwa na waasi.

Jeshi la Syria limekuwa likisaidiwa na ndege za kivita za Urusi kupambana na waasi hao tangu mwezi Septemba mwaka 2015.