SYRIA

Baraza la Usalama kukutana kwa dharura kujadili mashambulizi mjini Allepo

Msichana mdogo akitembea juu ya majengo yaliyoshambuliwa
Msichana mdogo akitembea juu ya majengo yaliyoshambuliwa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakutana baadaye siku ya Jumatano kujadili hali mbaya ya kibinadamu inayoshuhudiwa katika mji wa Allepo nchini Syria.

Matangazo ya kibiashara

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Staffan de Mistura anatarajiwa kuwaeleza wajumbe hao hali ya mambo katika mji huo ambao maeneo mengi kwa sasa, yanadhibitiwa na vikosi vya serikali.

Zaidi ya watu elfu 20 wameyakimbia makwao kwa muda wa saa 72 zilizopita kuepuka makabiliano kati ya waasi na wanajeshi wa serikali wanaosaidiwa na ndege za kivita za Urusi.

Kuelekea kwenye Mkutano huo, Umoja wa Mataifa umelaani mashambulizi katika mji huo na kusema wananchi wa kawaida ndio wanaoumia na hali ya kibinadamu ni mbaya.

Waangalizi wa Kimataifa wanasema kuwa uchunguzi wao wa hivi punde umesababisha zaidi ya watu 50,000 kuyakimbia makwao kwa muda wa siku nne zilizopita.

Watu 20,000 wamekimbilia Magharibi wa Allepo eneo ambalo kuna vikosi vya serikali huku watu wengine 30,000 wakikimbilia katika eneo ambalo kuna vikosi vya Kikurdi.