Nchi sita zenye nguvu duniani zatoa wito wa kusitisha mapigano Aleppo

Picha kwa juu ya mji mkongwe wa Aleppo iliyopigwa na ndege isiyo na rubani. Mbali kidogo eneo la kihistoria la mji wa Aleppo.
Picha kwa juu ya mji mkongwe wa Aleppo iliyopigwa na ndege isiyo na rubani. Mbali kidogo eneo la kihistoria la mji wa Aleppo. REUTERS/Abdalrhman Ismail

Kutokana na mashambulizi katika mji wa Aleppo yanayoendeshwa na vikosi vya serikali ya Syria dhidi ya waasi, nchi zinazounga mono upinzani nchini Syria zimeanza kulalamika.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, nchi hizi hazijakata tamaa kwa kuwa na matumaini ya kufikia makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano. Tayari Ufaransa na nchi nyingine tano za Magharibi, ikiwa ni pamoja na Marekani zimetoa wito wa kusitisha mapigano katika mji wa Aleppo.

Wito wa kusitisha mapigano katika mjo wa Aleppo umetolewa na sita zenye nguvu duniani ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Marekani, lakini pia Ujerumani, Italia, Uingereza na Canada. Awali nchi hizi sita zilidai mapigano yasitishwe mara moja, kutokana na hali ya kibinadamu inavyoshuhudiwa katikamji wa Aleppo na kulaani kwa kauli kali vitendo vya serikali ya Syria na washirika wake.

Ili kufikia makubaliano ya usitishwaji mapigano, nchi sita zimetishia kuchukua vikwazo vya ziada dhidi ya serikali ya Syria na wale wanaofanya kazi kwa niaba yake.

Wakati huo huo waasi nchini Syria wameondoka katika eneo kongwe la mji wa Aleppo baada ya kuelemewa na wanajeshi wa Syria wanaosaidiwa na ndege za kivita za Urusi.

Serikali ya Syria inasema hadi sasa inadhibiti asilimia 75 ya mji wa Allepo, mji ambao kwa miaka minne iliyopita, umekuwa chini ya waasi wanaomtaka rais Bashar Al Assad kuondoka madarakani. Hata hivyo, waasi wanasema hawawezi kuondoka katika mji huo.