SYRIA-IS-USALAMA

OSDH: shambulizi la kemikali karibu na mji wa Palmyra

Uharibifu mkubwa uliofanywa katika mji wa Palmyre.
Uharibifu mkubwa uliofanywa katika mji wa Palmyre. REUTERS/Omar Sanadiki

Shirika la Haki za Binadamu nchini Syria la OSDH limearifu kwamba kuna uwezekano kulitokea shambulizi la gesi Jumatatu hii katika eneo la linaloshikiliwa na wanajihadi wa kundi la Islamic state karibu na mji wa Palmyra, mji unaokumbwa na mashambulizi makali ya anga makali ambayo yalisababisha vifo vya watu 34.

Matangazo ya kibiashara

Likitoa mfano wa vyanzo vya karibu na eneo la mashambulizi katikamkoa wa mashariki wa Hama, kaskazini magharibi mwa mji wa Palmyra, OSDH imezungumzia visa ya kukosekana kwa hewa na watu kadhaa waliojeruhiwa wakati wa makombora yaliporushwa katika eneo hilo.

Vyanzo hivi vimebaini kwamba viliona miili ya watu waliouawa bila hata hivyo kuwa na majeraha, OSDH imeongeza.

Shambulizi hili la gesi, lililoendeshwa kwa ndege, lilitokea karibu na mji wa Oukaïrabat, kwenye barabara kubwa inayoelekea kusini mwa mji wa Palmyra, limesema shirika la Haki za Binadamu nchini Syria la OSDH, bila kusema waliohusika na shambulizi hilo.

Amaq, chombo cha propaganda cha kundi la Islamic State, kimesema katika taarifa yake kwamba watu 20 walifariki na wengine 200 waliathirika kutokana na matatizo ya kupumua "kwa sababu ya shambulizi la anga la Urusi kwa kutumia gesi aina ya Sari."

Wapiganaji wa kundi la IS waliuteka mji wa Palmyre Jumapili siku ya Desemba 11, licha ya mashambulizi ya anga yaliyoendeshwa na ndege za Urusi katika hali ya kuwarudisha nyuma. Itakumbukwa kwamba kundi la IS liliondolewa katika mji huo wa kale mwezi Machi mwaka jana.

Jeshi la Syria sawa na jeshi la Urusi yamekataa kuwa yalitumia silaha za kemikali. Mwaka huu, utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa ulionyesha kuwa jeshi la Syria lilitumia gesi aina ya klorini katika mashambulizi yake dhidi ya wapiganaji, na kwamba kundi la IS pia lilitumia silaha za maangamizi wakati wa baadhi ya mashambulizi. Serikali ya Damascus ilifutilia mbali matokeo ya uchunguzi huo.