SYRIA-USALAMA

Syria: mashambulizi ya jeshi mjini Aleppo yako katika awamu yake ya mwisho

Wapiganaji wa kundi la waasi katika Alepo ya masharikDesemba, 19, 2016.
Wapiganaji wa kundi la waasi katika Alepo ya masharikDesemba, 19, 2016. REUTERS/Abdalrhman Ismail TPX IMAGES OF THE DAY

 Mashambulizi ya jeshi la Syria na washirika wake yameingia Jumatatu hii katika "awamu yake ya mwisho" katika mkoa wa Aleppo Mashariki, huku maelfu ya raia wakiendelea kukimbia wakati ambapo vikosi vya mwisho vya waasi vilikua vikiuzingira mji wa Aleppo kwa idadi ndogo.

Matangazo ya kibiashara

Utawala wa Bashar al-Assad umelidhibiti mapema Jumatatu hii asubuhi eneo kubwa la Sheikh Said, kusini mwa mji wa Aleppo, kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu nchini Syria la OSDH, wakati ambapo mashambulizi ya anga na mashambulizi ya ardhini yamekua yakilenga eneo moja linalodhibitiwa na waasi.

Aleppo mji mkuu wa zamani wa kiuchumi wa Syria, ulikuwailigawanyika katika makundi mawili tangu mwezi Julai, 2012, kati ya mashariki , eneo linaloshikiliwa na waasi na magharibi eneo lililoko chini ya udhibiti wa serikali.

 Mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP ambaye aliweza kusikia mashambulizi ya anga kutoka eneo la Magharibi, amesema masambulizi hayo ni makali.