Wakazi wa mji wa Aleppo wahamishwa

Mabasi yamewkwa tayari kwa kuwasafirisha waasi na familia zao kuwaondoa katika mji wa aleppo, Desemba 15, 2016.
Mabasi yamewkwa tayari kwa kuwasafirisha waasi na familia zao kuwaondoa katika mji wa aleppo, Desemba 15, 2016. REUTERS/Omar Sanadiki

Mabasi ishirini na magari ya wagonjwa kumi yanatumiwa katika zoezi la kuwahamisha wakazi wa mji wa Alepo nchini Syria kiwa ni pamoja na waasi pamoja familia zao, Waziri wa Ulinzi wa Urusi amebaini.

Matangazo ya kibiashara

Kufuatia makubaliano kati ya serikali na waasi, watu waliojeruhiwa na familia zao ndio wameanza kuondoka na kisha waasi na familia zaopamoja na "wanamgambo 250" wasiokuwa na silaha wanapinga serikali, kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi.

Aidha, chanzo hicho kimesema, watu waliojeruhiwa na wagonjwa kutoka Foua na Kefraya, vijiji viwili vinavyokaliwa na Mashia wengi ambavyo vinadhibitiwa nawaasi katika mkoa jirani wa Idleb, pia watahamishwa katika maeneo yanayoshikiliwa na serikali.

Wapiganaji 12000 na familia zao pia zoezi hilo linawahusu.

Kudhibitiwa kwa Aleppo na jeshi la serikali itakua pigo kubwa kwa waasi ambao walidhibiti sehemu ya mashariki ya mji wa pili wa Syria mwaka 2012, lakini leo wanajikuta wameangamizwa baada ya mashambulizi makali ya jeshi la serikali yaliyozinduliwa katikati mwa mwezi Novemba .

Rais wa Syria Bashar Al Assad anatazamiwa kuhutubia wananchi mjini Aleppo Alhamisi hii.