JORDAN-USALAMA

Shambulio dhidi ya polisi laua watu zaidi ya 7 Kerak

Eneo la kitalii katika mji wa Kerak, kusini mwa Jordan.
Eneo la kitalii katika mji wa Kerak, kusini mwa Jordan. Wikimedia/CC BY 3.0/Berthold Werner

Watu wasiopungua saba waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa nchini Jordan Jumapili Desemba 18. Kundi la waasi walishambulia makao makuu ya polisi katika mjini wa Karak kusini mwa Jordan.

Matangazo ya kibiashara

Polisi wanne waliuawa pamoja na mtalii mmoja kutoka Canada na raia wawili wa Jordan. Inaonekana kuwa washambuliaji walikimbilia katika nyumba moja katika mji huo.

ikosi maalum vimetumwa katika eneo la tukio ili kusaidizana na vikosi vya usalama katikati mwa mji. Mji karibu wote umezingirwa. Wakazi wametakiwa kusalia nyumbani.

washambuliaji walishambulia kwa bunduki dhidi ya makao makuu ya polisi, katikati mwa mji wa Karak mnamo saa 7 mchana saa za Jordan,karibu na mneo la kitalii. Walishambuliwa magari mawili madogo ya polisi waliokua wakipiga doria katika mji wa Kerak.

Hakuna taarifa yoyote kuhusu kwa shambulizi hili. Vikosi vya usalama vinasema kuwa ni shambulio la kigaidi. Lakini walioendesha shambulizi hili hawajajulikana na sababu za shambulio lenyewe lililoendeshwa na watu 10. Kinachojulikana tu ni kwamba walikua walibebea silaha za kivita. na walikata kujisalimisha.

Shambulio kama hilo lilifanyika mwezi Juni katika kituo cha Idara ya upelelezi karibu na mji wa Amman, na kusababisha vifo vya watu watano.