UN-SYRIA

UN kupiga kura kuhusu kusimamia zoezi la kuwaondoa wakazi wa mji wa Aleppo

Mabaki ya hoteli Carlton katika mji wa Aleppo, katika eneo linalodhibitiwa na serikali ya Syria.
Mabaki ya hoteli Carlton katika mji wa Aleppo, katika eneo linalodhibitiwa na serikali ya Syria. REUTERS/Omar Sanadiki

Waasi 350 na familia zao waliweza kuondoka katika eneo la mashariki ya mji wa Aleppo, katika usiku wa Jumapili hadi leo Jumatatu baada ya tofauti kati ya makundi ya waasi ambazo zimesababisha kusimamishwa mchana kutwa wa siku ya Jumapili, kwa mkataba mpya wa zoezi hilo.

Matangazo ya kibiashara

Mjini New York, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeafikiana Jumapili jioni juu ya nakala yanayorejelea masharti ya azimio la Ufaransa kuhusu kutumwa kwa waangalizi mjini Aleppo. Kura inatarajiwa kupigwa leo Jumatatu.

Siku ya Jumapili usiku, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliafikiana juu ya rasimu ya azimio kuhusu usimamizi wa Umoja wa Mataifa wa zoezi la kuwaondoa wakazi na waasi katika mji wa Aleppo. Kura natarajiwa kupigwa leo Jumatatu asubuhi. Nakala hiyo inapanga kutumwa kwa waangalizi katika mji wa Aleppo kusimamia zoezi la kuwaondoa wakazi na waasi katika mji huo na zoezi la kutoa misaada ya kibinadamu, kwa mujibu wa wanadiplomasia.

Balozi wa Ufaransa François Delattre ameviambia vyombo vya habari kuwa nchi 15 wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wameafikiana kuhusu nakala ya maelewano, mwenzake wa Urusi Vitaly Churkin amebaini kuwa "Nakala hiuo ni nzuri". Wakati ambapo awali alikua alizungumza kwamba Urusi itapinga kwa kura ya turufu kuhusu rasimu ya azimio la kibinadamu lililotolewa na Ufaransa.

Mazungumzo yalikuwa magumu lakini wanadiplomasia waliwaonya hawataondoka bila ya makubaliano kwa minajili ya kuwaokoa raia katika mji wa Aleppo.

"Kianzio muhimu"

"Mkataba huu, ikiwa utathibitishwa, utakuwa kwa ufafanuzi kianzio, lakini kianzio muhimu sana, amesema François Delattre. Ni mara ya kwanza katika kipindi cha miezi kadhaa, baada ya ukusanyaji wa kura ambazo zilishuhudiwa, Baraza la Usalama kukubaliana, " amesema Balozi Delattre.