MAREKANI-ISRAEL-PALESTINA

Donald Trump aomba Marekani kutumia kura yake ya turufu kwenye rasimu ya UN

Askari wa Israel wakimkagua Mpalestina katika mji wa al-Fawar, Ukingo wa Magharibi Agosti 16, 2016.
Askari wa Israel wakimkagua Mpalestina katika mji wa al-Fawar, Ukingo wa Magharibi Agosti 16, 2016. AFP

Rais Mteule wa Marekani ameomba nchi yake kutumia kura yake ya turufu kwenye rasimu ya azimio la Umoja wa Mataifa dhidi ya coloni za Israel. Azimio hilo litaagiza kwamba shughuli zote za makaazi hayo katika eneo hilo la Palestina, ikiwemo Jerusalem mashariki lazima zisitishwe.

Matangazo ya kibiashara

Marekani imekuwa ikiunga mkono Israel katika Umoja wa Mataifa, lakini wanaounga mkono azimio hilo wamekuwa wakiamini kwamba utawala wa rais Obama utasusia kura hiyo.

"Kama Marekani inavyosema kwa muda mrefu, amani kati ya Waisrael na Wapalestina inaweza kupatikana tu kutoka mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili, na wala si kwa njia ya masharti yanayotolewa na Umoja wa Mataifa," amesema rais mteule wa Marekani. "Marekani inapaswa kutumia kura yake ya turufu kwenye azimio lililojadiliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa," Bw Trump ameomba, wakati ambapo kura ilikua inatarajiwa Alhamisi hii saa 9h alaasiri mjini New York. Rasimu ya azimio inadai kwamba Israel iache shughuli zake za ukoloni katika maeneo ya Palestina na katika Jerusalem ya Mashariki.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuishawishi Israel kusitisha ujenzi wa makaazi ya Israel katika ardhi ya Palestina.

Katika taarifa iliotolewa kabla ya kura hiyo inayotarajiwa baadaye siku ya Alhamisi, Bw Trump amesema kuwa amani haitaafikiwa kupitia hatua ya Umoja wa Mataifa kuweka masharti.

Marekani imekuwa ikiunga mkono Israel katika Umoja wa Mataifa, lakini wanaounga mkono azimio hilo wamekuwa wakiamini kwamba utawala wa rais Obama utasusia kura hiyo.