SYRIA-USALAMA

Jeshi la Syria latangaza kuurejesha kwenye himaya yake mji wa Aleppo

Kundi la mwisho la waasi na familia zao waondoka katika mji wa Aleppo Alhamisi hii Desemba 22.
Kundi la mwisho la waasi na familia zao waondoka katika mji wa Aleppo Alhamisi hii Desemba 22. Reuters/路透社

Jeshi la Syria limesema Alhamisi hii jioni kwamba liliurejesha kwenye himaya yake mji wa Aleppona kurejesha usalama katika mji huo baada ya kuondoka kwa kundi la mwisho la waasi.

Matangazo ya kibiashara

Kundi la mwisho la wapiganaji wa waasi na familia zao ambao walikuwa walijificha katika baadhi ya maeneo waliondolewa Alhamisi hii kama sehemu ya mkataba unaolipa jeshi na washirika wake udhibiti wa jumla wa mji huo, Runinga ya serikali imearifu.

jeshi la Syria lilitoa tangazo rasmi Alhamisi hii baada ya kuondolewa kwa kundi la mwisho la waasi kutoka katika Aleppo Mashariki, ngome ya zamani ya waasi iliyoanguka mikononi mwa jeshi la serikali baada ya mwezi mmoja wa mashambulizi ya angani na ya nchi kavu.

"Uongozi wa vikosi vya kijeshi utangazakurejea kwa usalama katika mji wa Aleppo baada ya kuachiwa kutoka kwa ugaidi na magaidi na kuwaondoa wale (...) ambao walikua wamebaki," ilisema taarifa ya jeshi iliyousomwa na afisa wa ngazi ya juu jeshini kwenye runinga ya serikali.