PALESTINA-ISRAEL-MAREKANI

Israel-Palestina: Netanyahu amshtumu John Kerry kwa matamshi yake

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry (kushoto) akizungumza na Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Tel-Aviv.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry (kushoto) akizungumza na Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Tel-Aviv. REUTERS/Pool

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry, wamejibizana vikali kuhusu azimio lililopitishwa hivi karibuni, kuizuia Israel kuendeleza ujenzi Mashariki mwa mji wa Jerusalem.

Matangazo ya kibiashara

Kerry amefafanua kuwa Marekani haikutumia kura yake ya veto kupinga azimio hilo kwa sababu ya kile inachoamini lakini akasisitiza kuwa ujenzi huu unahatarisha juhudi za upatikanaji wa amani kati ya Palestina na Israel.

Netanyahu kwa upande wake amesema matamshi ya Kerry yameegemea upande mmoja, na amesikitika kwa Kerry kutoa matamshi hayo kuhusu ujenzi wa makaazi hayo.

Uhusiano kati ya Netanyahu na rais Barack Obama, umekuwa ukidorora kuhusu mzozo wa Palaestina na Israel hasa kipindi hiki Obama anapotarajiwa kumaliza muda wake baadaye mwezi Januari.

Netanyahu amesema ana imani Israal itakuwa na uhusiano mzuri na uongozi wa Donald Trump.