PALESTINA-ISRAEL-MAREKANI

Mahmoud Abbas amuandikia Donald Trump akimuonya

Ahadi ya Donald Trump yakuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli inamtia wasiwasi Mahmoud Abbas.
Ahadi ya Donald Trump yakuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli inamtia wasiwasi Mahmoud Abbas. REUTERS/Issam Rimawi/Pool/File Photo

Hii ni moja ya ahadi za kampeni za Donald Trump. Rais mteule wa Marekani aliahidi kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli na kusema kuwa ataweka ubalozi wake katika mji huo, ambao kwa sasa unapatikana katika mji wa Tel Aviv.

Matangazo ya kibiashara

Ahadi hii iliyorejelewa mara kwa mara na watu walio karibu Donald Trump na sasa imeanza kuwatia wasiwasi Wapalestina wanaodai kuwa sehemu ya mashariki ya mji huo itakua mji mkuu wa Palestina. Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, amemuandikia Donald Trump akimuonhya kwa hilo.

Sera ya kigeni ya Donald Trumpimekua ikikosolewa na waangalizi wengi. Lakini kwa upande wa Wapalestina, ahadi zilizotolewa na Donald Trump zinatisha. Na wana hofu kwamba huenda mabadiliko hayo yakaanza kutekelezwa tangu Januari 20, baada ya Donal Trump kuchukua hatamu ya uongozi.

"Tulionywa kwamba rais Trump, katika hotuba yake ya kuapishwa, anaweza kuomba kuondolewa kwa ubalozi katika mji wa Tel Aviv na kuhamishwa katika mji wa Jerusalem, " amesema Mohamed Shtayyeh, mshauri wa karibu wa rais wa Palestina Mahmoud Abbas.

Mkataba wa Jerusalem unaweza kusainiwa katika makubaliano ya mwisho ya amani, Wapalestina wamekumbusha. Katika barua yake kwa Donald Trump, Mahmoud Abbas ameonya dhidi ya matokeo mabaya endapo uamuzi huo iutachukuliwa. Matokeo ambayo yanaweza kuwa mabaya zaidi, ameonya Mohamed Shtayyeh. "Hatutakubali na tutakataa kujadili suala hilo. Zaidi ya hayo, tutachukua hatua, "Bw Shtayyeh ameongeza.

Wapalestina pia wanategemea msaada wa nchi nyingine za Kiislamu ambao wanaamini kuwa Jerusalem ni mji takatifu. Mahmoud Abbas pia aliandikia wakuu wa nchi za Kiarabu kuwaomba kuingilia kati na kumsihi Donald Trump. Mamlaka ya Palestina pia imeitoa wito kwa Misikiti yote duniani kulaani uamuzi huo wakati wa sala tukufu ya Ijumaa wiki hii.