Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-UJUENZI

Israel yatangaza kujenga makaazi 3000 Ukingo wa Magharibi

Makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika mji wa Maale Edumin katika Ukingo wa Magharibi, Desemba 28, 2016.
Makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika mji wa Maale Edumin katika Ukingo wa Magharibi, Desemba 28, 2016. REUTERS/Baz Ratner
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Serikali ya Israel imetengaza mipango ya kujenga nyumba zaidi ya 3000 katika eneo la Ukingo wa Magharibi. Hata hivyo Mamlaka ya Palestina imepinga mipango hiyo ikiishtumu Israel kutaka kushikilia kimabavu maeneo ya Palestina. Baadhi ya viongozi duniani wamepinga mipango hiyo ya Israel.

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni serikali ya Israel iliidhinisha ujenzi wa nyumba 2500 katika Ukingo wa magharibi na nyengine zaidi ya 100 mashariki mwa Jerusalem.

Mamlaka ya Palestina imekua ikidai kuwa maeneo yote mawili ni sehemu ya ardhi ya Palestina.

Walowezi waliokuwa wamejenga katika ardhi ya Palestina walipewa makataa ya saa 48 kuondoka, jambo ambalo halikufanyika.

Jeshi la Israel lilikuwa likijiandaa kutekeleza operesheni ya agizo la mahakama ya kuwandoa.

baadhi ya viongozi duniani wamepinga mipango hiyo ya Israel ya kujenga makaazi katika maeneo ya Palestina.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.