MAREKANI-ISRAEL-PALESTINA

Washington kutokubliana na makaazi mapya ya Israel nchini Palestina

Donald Trump hafurahishwi na upanuzi wa makaazi ya Israel katika maeneo ya Palestina.
Donald Trump hafurahishwi na upanuzi wa makaazi ya Israel katika maeneo ya Palestina. Reuters

Ikulu ya White House imetangaza kwamba haikubaliani na ujenzi wa makaazi mapya ya Israel katika maeneo ya ardhi ya Palestina. Donald Trump ametangaza hadharani katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Alhamisi hii Februari 2.

Matangazo ya kibiashara

"Kuwepo kwa makazi si kikwazo kwa amani. Lakini ujenzi wa makazi mapya au upanuzi wa maeneo yaliokuwepo nje ya mipaka yao inaweza kutosaidia kufanikisha lengp hili, " kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu ya Marekani.

Waziri Mkuu Netanyahu, kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari vya Marekani, amekosea. Hakuitaarifu Marekani kabla ya kuchukua uamuzi wa kujenga makaazi mapya.

Taarifa hii pia inasema kuwa utawala wa Trump haijawa na msimamo rasmi kuhusu "shughuli makaazi mapya ya Israel nchini Palestina." Vile vile, hoja iliyotangazwa na Marekani ya kuhamishwa kwa ubalozi wa Marekani katika mji wa Jerusalem imehirishwa.

Hii ni nji pekee ya kuonyesha kuwa Marekani ina mchango mkubwa katika kutafutia suluhu mzozo kati ya Israel na Palestina, na kutovunjika kwa uhusiano kati ya Marekani na Israel. Rais wa Marekani anamsubiri Benjamin Netanyahu Februari 15 mjini Washington.