Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-UJENZI

Israel kuendelea na mpango wake wa ujenzi wa makaazi katika Ukingo wa Magharibi

Wabunge wa Israel wapitisha muswada ambao unaruhusu Israel kuchukua mamia ya hekta za ardhi ya Palestina katika Ukingo w Magharibi, Jumatatu, Februari 6, 2017.
Wabunge wa Israel wapitisha muswada ambao unaruhusu Israel kuchukua mamia ya hekta za ardhi ya Palestina katika Ukingo w Magharibi, Jumatatu, Februari 6, 2017. REUTERS/Ammar Awad
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Bunge nchini Israel, limepitisha sheria tata kuhusu ujenzi wa makaazi mapya ya walowezi katika Ukingo wa Magharibi. Sheria hiyo imepitishwa na wabunge 60 huku 52 wakipinga.

Matangazo ya kibiashara

Kura hii ilioahirishwa siku chache kabla, hatimaye imefanyika katika usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne Februari 7. Bunge la Israel (Knesset) limepitisha sheria ambayo itaruhusu Israel kuchukua mamia ya hekta za ardhi ya Palestina katika ukingo wa Magharibi kwa ajili ya ujenzi wa Makaazi 4000.

"Sheria hii mpya ya Israel inahalalisha wizi wa ardhi ya Palestina. ". Ni katika maneno haya chama kilichoanzishwa na Yassir Arafat cha PLO kimeonya. PLO ilionya kabla ya kura hiyo kwamba inaona katika Nakala hiyo "tangazo la vita".

Wamiliki wa ardhi katika eneo hilo ambalo Wapalestina wanadai ni lao watapewa fidia kwa mujibu wa sheria hii mpya, ili kutoa nafasi ya kujenga makaazi mapya elfu nne.

Hatua hii inakuja baada ya polisi wa Israel kuwaondoa kwa nguvu watu waliokuwa wanaishi katika eneo la Amona, ambalo ni eneo la Palestina na kuahidiwa kupewa hifadhi katika eneo la ukingo wa Magharibi.

Serikali ya Mamlaka ya Palestina imelaani hatua hii na kusema kuwa, itaendelea kuzua hali ya wasiwasi kati yake na Israel na kuendelea kudidimia matumaini ya kupata amani ya kudumu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.