UTURUKI-URUSI-SYRIA-USALAMA

Uturuki yawapoteza askari 3 katika mashambulizi ya Urusi nchini Syria

Askari watatu wa Uturuki wameuawa Alhamisi hii katika mashambulizi ya angani ya Urusi yaliyoendeshwa kaskazini mwa Syria, jeshi la Uturuki limetangaza.

Askari wa Uturuki Septemba 2, 2016 katika mji wa Jarabulus nchini Syria kwenye mpaka na Uturuki.
Askari wa Uturuki Septemba 2, 2016 katika mji wa Jarabulus nchini Syria kwenye mpaka na Uturuki. AFP
Matangazo ya kibiashara

Askari wengine kumi na mmoja wa Uturuki wamesalimika katika mashambulizi hayo. Wakati huo huo rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa rambirambi zake kwa mwenzake wa Uturuki Tayyip Erdogan, jeshi la Uturuki limeongeza katika taarifa yake.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ndege za Urusi zimekua zikijaribu kulenga kundi la la wanajihadi. "Askari watatu wamepoteza maisha kama mashujaa wakati jengo ambamo askari hao waliokuemo lililposhambuliwa."

Taarifa hiyo haikutaja ni eneo gani la kaskazini mwa Syria kulikotokea tukio hili.

Rais wa Urusi ameonyesha "huzuni zake na kutoa rambirambi zake, " taarifa ya kijeshi imebaini.

Mjini Moscow, Ikulu ya Kremlin imetangaza kwamba marais Putin na Erdogan wamekengeuka katika mazungumzo haya ya simu ya kuimarisha ushirikiano dhidi kundi la Islamic State.

Vyombo vya habari vya Uturuki vimearifu mapema kwamba askari wengine watano wa Uturuki wameuawa Alhamisi hii katika vita dhidi ya wanajihadi wa kundi la IS kaskazini mwa Syria, ambapo askari wengi wa Uturuki wameuawa katika eneo hili ndani ya siku mbili.