MAREKANI-ISRAEL-USIRIKIANO

Donald Trump kukutana kwa mazungumzo na Benjamin Netanyahu

Donald Trump pamoja na Benjamin Netanyahu wakati wa mkutano wao mjini New York Septemba 25, 2016.
Donald Trump pamoja na Benjamin Netanyahu wakati wa mkutano wao mjini New York Septemba 25, 2016. Kobi Gideon/Government Press Office (GPO)/Handout via REUTERS

Rais wa Marekani, Donald Trump baadae hii leo atamkaribisha kwenye ikulu ya Washington, waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, wakati huu afisa wa Trump akigusia kuwa Marekani haitasisitiza tena suala la suluhu ya nchi mbili kati ya Israel na Palestina.

Matangazo ya kibiashara

Marekani sasa inaonekana kuwa haitashiriki kuelekeza namna yoyote ya kutafuta suluhu kwenye mzozo wa Israel na Palestina, lakini itaunga mkono chochote ambacho kitakubaliwa na pande hizo mbili.

Awali Rais Donald Trump aliunga mkono Israel kujenga makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Palestina, lakini siku chache baadae alifutilia mbali mpango huo.

Trump amekua akikosolewa kwa maamuzi yake, ambayo wadadisi wanasema yamekua yakichukuliwa bila hata hivyo kuwa na imani kuwa yanaweza kuleta madhara makubwa na kusababisha hali ya mvutano kati ya raia wa Marekani au hata kati ya Marekani na washirika wake.