MAREKANI-ISRAEL-PALESTINA

Trump atoa sera ya Marekani kuhusu suluhu kwa Israel na Palestina

Rais wa Marekani Donald Trump amesema, uongozi wake unaunga mkono uundwaji wa taifa moja kumaliza mzozo wa Israel na Palestina.

Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kabla ya mkutano wao katika Ikulu ya Marekani Februari 15, 2017.
Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kabla ya mkutano wao katika Ikulu ya Marekani Februari 15, 2017. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Trump amesema hili na kuonekana kubadilisha sera ya Marekani ya muda mrefu ya kutaka Israel na Palestina kuwa mataifa mawili tofauti yanayoishi kwa amani.

Donald Trump amesema pande zote mbili zitahitajika kuwa na maridhiamo, na kwamba angetaka Israel isitishe kidogo ujenzi wa makazi unaoendelea.

Kwa upande wake, bwana Netanyahu amesema Israel inapaswa ihakikishe kuwepo kwa usalama katika eneo linalokaliwa la Ukingo wa Magharibi.

Bwana Netanyahu pia amesema anaamini kwamba uongozi wa bwana Trump unatoa fursa ya kihistoria ya kubadilisha kile alichokiita kama kuwepo kwa wimbi la waislamu wenye msimamo mkali.

Rais Trump pia amemwambia mgeni wake kuwa, atahakikisha kuwa mkataba wa amani unapatikana.

Isreal na Palestina hazijazungumza tangu mwaka 2014.