SYRIA-USALAMA

Baada ya miaka 2 ya utulivu, mapigano yaanza karibu na Damascus

Nchini Syria, hali ya utulivu ilikua imeshuhudiwa kwa miezi mjini Damascus na kusini mwa nchi lakini kwa sasa mapigano yameanza katika maeneo hayo siku chache ya kabla ya mazungumzo ya amani mjini Geneva, yaliyopangwa Februari 23 chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa.

Katika kata ya Douma, karibu na Damascus, Februari 19, 2017.
Katika kata ya Douma, karibu na Damascus, Februari 19, 2017. REUTERS/Bassam Khabieh
Matangazo ya kibiashara

Baada ya miaka miwili ya utulivu, milio ya risasi na milipuko ya mabomu vimeanza kusikika katika kata ya Qaboun, kaskazini mashariki mwa Damascus. Mapigano hayo mpaka sasa yamesababisha vifo vya watu 16 tangu Jumamosi Februari 18, kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu nchini Syria la OSDH.

mapigano hayo yanaongezeka wakati ambapo idadi kubwa ya jeshi ikiendelea kutumwa katika uwanja wa mapigano nchini Syria. Shirika la Haki za Binadamu nchini Syria la OSDH na vyombo vya habari vilio karibu na serikali ya Damascus vimebaini kwamba kunashuhudiwa operesheni kabambe ya kijeshi kwa lengo la kuwatimua waasi pembezoni mwa mji mkuu. Gazeti la kila siku la Al-Watan linalounga mkono serikali limearifu kwamba ujumbe wa kijeshi wa maafisa wa Syria na washauri wa kijeshi wa Urusi walifanya ziara ya ukaguzi katikauwanja wa kivita, kabla ya kuanza kwa mapigano.

Katika mji wa Deraa kusini mwa Syria, mapigano makali yanaendelea baada ya waasi na wapiganaji wa kijihadi kuzindua mashambulizi dhidi ya sehemu ya mji inayodhibitiwa na serikali. pamoja na msaada wa mashambulizi ya angani ya ndege za Urusi na zile za Syria , mashambulizi ya wapiganaji yamedhibitiwa; lakini jeshi la Syria bado halijaweka kwenye himaya yake ngome ilizopoteza.

Pia mapigano yanaendelea katikati mwa Syria kati ya jeshi na kundi la Islamic State. Wanajeshi wa serikali wanasonga mbelekatika maeneo kadhaa ya jangwani na wamefikia kilomita 18 kutoka mji wa kale wa Palmyra.