IRAQ-USALAMA

Vikosi vya Iraq lakabiliana na IS katika uwanja wa ndege wa Mosul

Operesheni ya kuwatimua wapiganaji wa kundi la IS kutoka Mosul ilianza Jumapili Februari 19, 2017.
Operesheni ya kuwatimua wapiganaji wa kundi la IS kutoka Mosul ilianza Jumapili Februari 19, 2017. REUTERS/Zohra Bensemra

Jeshi la Iraq limezingira uwanja wa ndege wa Mosul katika mapambano dhidi ya kundi la Islamic State. Raia wa maeneo ya mji huo wana hofu ya kupoteza maisha iwapo mapigano yatazuka.

Matangazo ya kibiashara

Haya ni mapambano ya mwezi wa nne sasa katika harakati za kuwaondoa wapiganaji hao katika mji huo.

Jeshi la Iarq mwishoni mwa wiki iliyopita, lizindua operesheni maalum ya kupambana na magaidi hao, huku mamia ya magari ya kijeshi yakionekana katika mji huo.

Hofu ni kwa zaidi ya watu zaidi ya Laki saba amba wanaishi katika mji huo, kwa sababu huenda wakaangamia au kujeruhiwa watakapokuwa wanakimbia mapigano hayo.

Ikiwa jeshi la Iraq, litafanikiwa kuuchukua mji wa Mosul, litakuwa ni pigo kubwa sana kwa Islamic State ambao wamekuwa wakidhibiti mji huo toka mwaka 2014.