SYRIA-IS-USALAMA

Jeshi la Syria laingia Palmyra, nchini Syria

Uharibifu wa kundi la IS katika mji wa kale wa Palmyra, Machi 27, 2016.
Uharibifu wa kundi la IS katika mji wa kale wa Palmyra, Machi 27, 2016. AFP

Vikosi vya serikali ya Syria vimeingia Jumatano jioni wiki hii katika mji wa kale wa Palmyra baada kupambana na wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS) linalodhibiti mji huu ulio katikati mwa nchi, shirika moja la kiserikali limebaini.

Matangazo ya kibiashara

"Jeshi la Syria limeingia katika eneo la magharibi la mji Palmyra na limechukua udhibiti wa moja ya sehemu mji huo," Mkurugenzi wa shirika la Haki za Binadam nchini Syria la (SOHR), Rami Abdul Rahman.

"Kuna mapigano na mashambulizi makali ya angani katika mji wa Palmyra," Bw Abdul Rahmani ameongeza.

Mapema, Rami Abdel Rahman alisema kuwa vikosi vya Syria viko nje kidogo ya mji.

Vikosi vya serikali ya Syria vimekua vikijaribu kwa wiki kadhaa kuudhibiti mji wa Palmyra vikipitia katika mkoa wa Homs, baada ya kusaidiwa na mashambulizi ya angani na vikosi vya nchi kavu vya Urusi.

Kundi la Islamic State liliudhibiti mji wa Palmyra mwezi Maei 2015, na wapiganaji wake waliharibu mahekalu mazuri na kuwaua raia kadhaa katika sehemu hizo.

Wapiganaji hao walitimuliwa katika mji huo wa kale mwezi Machi 2016 lakini waliudhibiti tena mwezi Desemba 2016.