SYRIA-IS-USALAMA

Jeshi la Syria laudhibiti mji wa kale wa Palmyra

Mji wa kale wa Palmyra, pamoja na bango linalowaelekeza watalii, Syria, Machi 27, 2016, baada ya serikali kuudhibiti mji huo kutoka mikononi mwa kundi la IS.
Mji wa kale wa Palmyra, pamoja na bango linalowaelekeza watalii, Syria, Machi 27, 2016, baada ya serikali kuudhibiti mji huo kutoka mikononi mwa kundi la IS. STRINGER / AFP

Jeshi la Syria likisaidiwa na ndege za kivita za Urusi limefanikiwa kuchukua mji wa kihistoria wa Palmyra kutoka kwa wapiganaji wa kiislamu wa Islamic State.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu, amemtaarifu rais Vladmir Putin kuhusu kutamatika kwa operesheni hiyo kwenye mji wa Palmyra, amesema msemaji wa utawala wa Moscow Dmitry Peskov.

Makundi ya waangalizi ambayo yamekuwa yakifuatilia vita hiyo, wameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP, kuwa wakati wanajihadi hao wakiondoka kwenye mji wa Palmyra, vikosi vya Serikali bado havijaingia kwenye mji huo.

"IS wameondoka kabisa kwenye mji wa Palmyra, lakini vikosi vya Serikali ya Syria bado vinaendelea na operesheni ya kusafisha miji jirani na bado hawajaingia kwenye mji wote," amethibitisha mkurugenzi wa shirika la haki za binadamu.

Mji huu kwa mara kadhaa umeshuhudia makabiliano ya mara kwa mara huku kila upande ukiwa umeshawahi kuushikilia mji huo, ambao maeneo yake mengi ya kihistoria yameharibia vibaya na wapiganaji wa IS.

Wanajihadi hao waliuchukua mji huo mwezi May 2015 na kuanza kuharibu maeneo yake ya kihistoria hasa maeneo ambayo yalikuwa yameorodheshwa na UNESCO kama urithi wa dunia.

Vikosi vya Serikali na Urusi vilifanikiwa kuwafurusha wanajihadi hao Marchi 2016 lakini walifanikiwa kuuchukua mji huo mwezi Desemba mwaka jana.