IRAN-IRAQ-SYRIA-USALAMA

Iran yatangaza vifo vya askari 2,100 waliotumwa nchini Iraq na Syria

Askari wa Iran wakibeba miili ya wapiganaji waliojitolea waliouawa Syria , Februari 6, 2016 mjini Tehran.
Askari wa Iran wakibeba miili ya wapiganaji waliojitolea waliouawa Syria , Februari 6, 2016 mjini Tehran. ATTA KENARE / AFP

Iran imetangaza vifo vya askari waliostaafu 2,100 wakiwemo wapiganaji waliojitolea ambao walitumwa nchini Iraq na Syria. Ni Jambo lisilo la kawaida viongozi wa Iran kutoka idadi ya vifo vya watu wao katika nchi hizi mbili, ambao imekua ikiwatuma washauri wa kijeshi na wapiganaji wanaokjitolea kusaidia majeshi ya Iraq na Syria.

Matangazo ya kibiashara

Idadi hii imetolewa na kiongozi wa chama cha maveterani wa vita na mashujaa wa kivita. "Askari 2,100 wakiwemo wapiganaji walikufa mashujaa nchini Iraq na mahali pengine kwa kutetea maeneo takatifu," amesema Mohammad Ali Shahidi.

Maeneo takatifu ni makaburi ya Maimamu kadhaa warithi wa Mtume Muhammad, kwa mujibu wa Waislamu kutoka dghehebu la Shia nchini Iran na Iraq, na watu kutoka familia ya Mtume.

Mwezi Novemba mwaka jana, kiongozi huyo alitangaza vifo vya wapiganaji 1000 waliotumwa na Iran nchini Syria. Iran inasaidia kifedha na kijeshi serikali za Iraq na Syria.

Serikali ya Tehran amekua ikiwatuma washauri wa kijeshi lakini pia wapiganaji "wanaojitolea" kutoka Iran, au Afghanistan na Pakistan katika nchi hizo mbili. Iran inasema zoezi la kutumwa askari hawa na wapiganaji wanaojitolea linafanyika kwa ombi la serikali za Syria na Iraq.

Miongoni mwa waliopoteza maisha, kulikuwa na maafisa kadhaa waandamizi waliostaafu katika kikosi cha Ulinzi wa Taifa, askari kutoka kikosi maalum cha utawala wa Kiislamu waliouawa nchini Syria katika miaka ya hivi karibuni.