SYRIA-MAREKANI-URUSI-UTURUKI-USHIRIKIANO

Syria: Mkutano wa kijeshi kati ya Washington na Moscow

Wakuu watatu wamajeshi,Hulusi Akar kutoka Uturuki (katikati), Joseph Dunford kutoka Marekani (kushoto) na Valery Gerasimov kutoka Urusi (kulia) Machi 7, 2017 Antalya (kusini mwa Uturuki).
Wakuu watatu wamajeshi,Hulusi Akar kutoka Uturuki (katikati), Joseph Dunford kutoka Marekani (kushoto) na Valery Gerasimov kutoka Urusi (kulia) Machi 7, 2017 Antalya (kusini mwa Uturuki). AFP

Jumanne wiiki hii Wakuu wa majeshi ya Uturuki, Marekani na Urusi walijadili njia za kuboresha uratibu wao nchini Syria ili kuepuka mapigano baina ya majeshi kutoka nchi hizo ambapo nchi zao zinaunga mkono dhidi ya kundi la Islamic State (EI).

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu wa kipekee uliozishirikisha nchi tatu umefanyika wakati ambapo serikali ya Ankara inapinga kushiriki katika operesheni za wanamgambo wa Kikurdi wanaoungwa mkono na Marekani. Wakati huo huo kundi la IS limedhoofika kutokana na mashambulizi ya muungano wa kimataifa ndhi ya wanajihadi unaoongozwa na Marekani pamoja na vikosi vinavyoungwa mkono na Urusi.

Mvutano unaendelea kushuhudiwa katika mji wa Syria wa Minbej, ambapo Uturuki inataka kuwatimua wanamgambo wa Kikurdi wa YPG, lakini Marekani na Urusi wamechukua hatua ya kukatisha tamaa serikali ya Ankara kuchukua hatua peke yake bila kushirikisha wengine.

Maafisa watatu wa kijeshi, Hulusi Akar kutoka Uturuki, Joseph Dunford kutoka Marekani na Valery Gerasimov kutoka Urusi walikutana Jumanne wiki hii katika mji wa Antalya (kusini mwa Uturuki) na wanatazamiwa kukutana tena Jumatano wiki hii, amesema Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yildirim.

"Tunatakiwa kuratibu vizuri, kwa sababu kuna nchi nyingi pale (nchini Syria) (...) Kama hakuna uratibu huo, kunaweza kukatokea hatari ya mapambano, " Bw Yildirim amesema.

"Ni vizuri kuyaepuka (...) kama pande tofauti zitashirikiana katika shughuli za wengine, na kuhakikisha kwamba matukio ya kusikitisha hayatokei, " ameongeza kiongozi wa serikali ya Uturuki.