AFGHANISTAN-IS-USALAMA

Watu zaidi ya 30 wauawa katika shambulizi la IS mjini Kabul

Polisi wa Afghanistan wakiwasili katika eneo la mashambulizi dhidi ya hospitali kuu ya kijeshi nchini Afghanistan, katikati mwa mji wa Kabul, tarehe 8 Machi 2017. Shambulio ambalo linadaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State (IS), lilidumu masaa sita.
Polisi wa Afghanistan wakiwasili katika eneo la mashambulizi dhidi ya hospitali kuu ya kijeshi nchini Afghanistan, katikati mwa mji wa Kabul, tarehe 8 Machi 2017. Shambulio ambalo linadaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State (IS), lilidumu masaa sita. REUTERS/Omar Sobhani

Hospitali kubwa ya kijeshi katika mji wa Kabul, nchini Afghanistan imelengwa na shambulizi Jumatano hii, Machi 8. Baada ya masaa sita ya milio ya risasi, mapigano kati ya majeshi ya Afghanistan na washambuliaji, waliojifananisha na madaktari, "yamemalizika" kwani wahusika wote wa shambulio "wameuawa," kwa mujibu wa Idara za usalama.

Matangazo ya kibiashara

Kundi la Islamic State limedai kuhusika na shambulizi hilo lililogharimu maisha ya watu zaidi ya 30 na kuwjeruhi wengine kadhaa, kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni kutoka Wizara ya Afya.

Zaidi ya watu 30 wameuawa, kulinga na maafisa, lakini baadhi ya ripoti zinasema kuwa idadi ya vifo huenda ikawa kubwa zaidi.

Kundi la Taliban limekanusha kuhusika, kulingana na ripoti ya vyombo nchini humo.

Polisi wa Afghanistan wakiwa katika eneo la shambulio, mjini Kabul.
Polisi wa Afghanistan wakiwa katika eneo la shambulio, mjini Kabul. REUTERS/Omar Sobhani

Rais Ashraf Ghani amesema kuwa shambulio hilo kwenye hospitali ya Sardar Daud, hospital yenye uwezo wa kuwalaza wagonjwa 400 ni "uvunjaji wa maadili yote ya binadamu".

" Katika dini zote, hospitali inachukuliwa kama mahala penye kinga na kuishambulia ni kuishambulia Afghanstan nzima ," alisema.

IS wamekuwa wakiendesha harakati zao nchini Afghanistan tangu mwaka 2015 na tayari wamekwisha tekeleza mashambulizi kadhaa nchini humo.