SYRIA-IRAQ

Zaidi ya watu 50 wauawa jijini Damascus

Takribani watu Hamsini na tisa wameuawa na wengine zaidi ya mia moja kujeruhiwa katika milipuko miwili iliyotokea jumamosi katika mashambulizi yaliyolenga raia jijini Damascus.

Mashambulizi katika mji wa Damascus yameua watu 59
Mashambulizi katika mji wa Damascus yameua watu 59 Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya ndani wa Syria Mohammed al-Shaar ametembelea majeruhi katika hospitali za jijini humo na kuthibitisha vifo hivyo na majeruhi.

Waangalizi wa haki za binadamu wanaarifu kuwa miongoni mwa waliouawa ni raia wa Iraq 47 na wapiganaji 12 wanaoung amkono serikali ya Syria.

Televisheni ya taifa la Syria imearifu watu 40 wameuawa na mia moja arobaini wamejeruhiwa baada ya magaidi kutekeleza mashambulizi mawili.